NEWS | 2017 ZAMU YA B-FACE | HIP HOP
![]() |
Picha na Isaac Classic |
Baada ya ku saini mkataba na management yake mpya ya TMG (Treibeka Music Group) mwaka huu mwanzoni, B-face ameonekana kushamiri kwenye muziki wa Hip Hop tangu baada ya ku achia wimbo wake ulio beba jina la LA DIFFERENCE, uliompa umaarufu mkubwa nchini Burundi na Rwanda.
GIRIKWISHAKA Boniface, B-Face hajaregeza mkanda wa hip hop wala kuliachia gurudumu hilo, Alifuatisha na wimbo SIPENDI UJINGA ambao umezidi kumjenga vilivyo na akamalizia na INGOMA ZIWACU ambapo ameonekana kuwa hajabahatisha.
Kwenye kipindi cha Ahabona moment kwenye Radio Colombe, amechaguliwa na wapenzi wa muziki wa nyumbani kuwa kama mwana hip hop bora wa mwaka na kupewa tuzo ya heshima. hapo juzi tareh 29 Desemba 2017 jijini Bujumbura tarafani Mukaza, kata ya Jabe, amepewa tuzo na ku vishwa taji la heshima kama mwana hip hop bora wa mwaka, Jana pia tareh 30 Desemba kapewa Tuzo na cheti cha heshima kama msanii bora wa hip hop mwaka 2017.
![]() |
Picha na Isaac Classic |
Kitu hiki kimethibitishwa na watu wengi kuwa mwanamuziki huyu amefaa kunyakua tuzo hizi.
Ingoma ziwacu by B face
0 comments: