Picha na Isaac Classic



Baada ya ku saini mkataba na management yake mpya ya TMG (Treibeka Music Group) mwaka huu mwanzoni, B-face ameonekana kushamiri kwenye muziki wa Hip Hop tangu baada ya ku achia wimbo wake ulio beba jina la LA DIFFERENCEuliompa umaarufu mkubwa nchini Burundi na Rwanda.

GIRIKWISHAKA Boniface, B-Face hajaregeza mkanda wa hip hop wala kuliachia gurudumu hilo, Alifuatisha na wimbo SIPENDI UJINGA ambao umezidi kumjenga vilivyo na akamalizia na INGOMA ZIWACU ambapo ameonekana kuwa hajabahatisha.
Kwenye kipindi cha Ahabona moment kwenye Radio Colombe, amechaguliwa na wapenzi wa muziki wa nyumbani kuwa kama mwana hip hop bora wa mwaka na kupewa tuzo ya heshima. hapo juzi tareh 29 Desemba 2017 jijini Bujumbura tarafani Mukaza, kata ya Jabe, amepewa tuzo na ku vishwa taji la heshima kama mwana hip hop bora wa mwaka, Jana pia tareh 30 Desemba kapewa Tuzo na cheti cha heshima kama msanii bora wa hip hop mwaka 2017.

Picha na Isaac Classic

Kitu hiki kimethibitishwa na watu wengi kuwa mwanamuziki huyu amefaa kunyakua tuzo hizi.


Ingoma ziwacu by B face

0 comments:








Mabibi na mabwana Madiba The Classic ametusogezea hii hapa mpya yake.



0 comments:





Imeonekana leo mchana kwenye mitandao ya kijamii Clip video yenye sekunde 53 ya Natacha La Number akim'cover A flow kwenye wimbo wake La Number, Ni baada ya picha kem kem kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wakiwa sehemu za bustani A Flow akimcharazia kinanda aina ya Piano mwanadada Natacha siku ya jana.


Video inapatikana hapa chini


Tukumbuke kwamba mwanadada huyo ameahidi kumsaidia msanii huyo chipukizi A Flow kwa namna moja au nyingine, Na safari ya msaada ndio kama imeanza.

Swali ni kwamba "Natacha amegundua kitu gani kwa msanii huyo chipukizi?" wanajiuliza mashabiki wa muziki.






              

0 comments:



MANIRAMBONA IBRAHIM maarufu kama ICUBURUNDI, muigizaji anaetikisa tasnia ya filamu nchini Burundi, anaonekana kushamiri kwenye tasnia hii tangu baada ya filamu alioigiza na muigizaji wa kike kutoka nchini Tanzania, SHAMSA FORD, na kujipatia umaarufu mkubwa nchini nakujitangaza ki kazi nchini Tanzania ambako anaonekana mara nyingi kujielekeza huko kufanya kazi nyingine kem kem.

Tukumbuke ni mwaka jana ambapo waliweza kumleta muigizaji mwingine kutoka nchini Tanzania Hemedy Suleiman nakufanya nae Movie ambayo imepewa jina la BURUNDIAN IN DAR ila mpaka dakika hii haijajulikana ni lini itaachiwa.


Icuburundi kwasasa aliweza kuachia filamu mpya ambayo inatamba nchini GENDER EQUALITY, kama ulikua bado hujabahatika kuitazama hii hapa chini nimeikusogezea.



2 comments:



Baada ya kusikika FLOW SLIM kwenye wimbo wake LA NUMBER ambao inasikika kwamba alikua akimuagizia ujumbe msanii mwenzie NATACHA ambae inafahamika kwamba yupo tayari ndoani.


Leo hii al-khamisi 28 Disemba, 2017 majira ya saa tano asubuhi, zimeonekana picha kadhaa za wawili hao wakiwa sehemu kwenye bustani A flow akimcharazia kinanda Natacha kwa ishara ya kumuimbia wimbo.




Tukumbuke kwamba Natacha aliahidi kumuonyesha ushirikiano mkubwa msanii huyo ambapo hakuweza kufunguka ni aina gani ya ushirikiano...
Baada ya hapo alionekana A flow kwenye exclusive interview ya NGM TV SHOW alipoulizwa kuhusiana na wimbo huo amejibu kua ni hisia zake zaukweli dhidi ya Natacha kwa maana kwamba anampenda kwa dhati.



Kama umepitwa na interview hiyo hii hapa nimekusogezea



0 comments:







BUTOYI Bertin Maarufu kama Berry Prince ni mmoja kati ya wasanii wa Burundi wanaoishi na kuendeleza kazi zao za muziki huko nchini Australia, Ni kijana mashughuli anaejituma kufanya kazi nzuri ili kesho ajitangaze kimataifa.


Leo hii ametusogezea video yake mpya ya wimbo alioshirikiana na msanii mwenzie wa kike ambae ni Veronica, Hivo basi Burudika na video hii hapa chini





                 

0 comments:

                             


Msanii wa kizazi kipya nchini Burundi anaetamba kwa wimbo wa QU'EST CEQU'IL YA ( KESKILYA) aliomshirikisha Fizzo, Ndayisaba Junior a.k.a Mr. Champagne, Amedhihirisha wazi siku ya ijumaa pili tareh 24 disemba 2017 baada ya tamasha lililowakusanya wasanii kutoka Burundi Natacha na Vichou pamoja na msanii kutoka Jemhuri ya kidemokrasiya ya Congo Fally Ipupa, Licha ya msanii huyo Mr Champagne kuonekana kwenye picha nyingi akiwa na Fally Ipupa mitandaoni.





"Mimi ni shabiki wako mkubwa hapa Burundi" alitamka Mr Champagne akimuelezea role modele wake, kwa ku thibiti hilo Fally alimuimbia wimbo wake mmoja huku Mr Champagne aki mkatia mauno.

Hii hapa ni post alioweza kuipost siku ya jana kwenye ukurasa wake wa facebook.




  
               

0 comments:







Baada ya KINGORONGORO kutangaza kuwa hivi punde ataachia wimbo mpya kwa jina la VUNJA GOTI, Rapper huyo kwa muujibu wake andai sio wimbo wa kawaida, huku marappers wengine matumbo joto...


Habari tulizo nazo hapa ni kwamba kwenye wimbo huo ameshirikiana na Producer pia Msanii ambae ni KOLLY THE MAGIC, na wimbo huo utaachiwa AUDIO & VIDEO, ila bado hajatangaza ni lini atauruhusu.

Mashabiki wa muziki wa nyumbani wameanza kutumia jina la wimbo huo kama SLOGAN kwenye mitandao ya kijamii hata mitaani kwao pia ku dhihirisha ni jinsi gani wanavyo usubiri kwa hamu.

Tukumbuke kwamba ni hapo juzi tu ambapo msanii huyo alipoweza kuachia wimbo wake mpya kwa jina la KALI NA NUSU ambao haujachukua hata wiki mbili mara ghafla ametangaza atauachia wimbo mwingine.



                  

0 comments: