NEWS | NASAHA YA GAGA BLUE




Msanii wa muziki wa kizazi kipya Gaga Blue anaetamba kwa wimbo wake IVO IVO alioshirikiana na msanii kutoka Tanzania Young D, amewataka wasanii wa muziki wa Indundi Music  kuwekeza pesa za nyingi kwenye muziki wao ili kuongeza thamani ya muziki wa Burundi.

Muimbaji huyo ameiambia ( Rundiwood) kuwa uwekezaji kwenye muziki ndiyo siri ya kufanikiwa kwa wasanii wengi na ilo tayari ameligundua kwa wasanii wengi nchini Tanzania.


Aidha msanii huyo alitoa mfano kwake na kusema kuwa mara nyingi anawekeza sana bila kujali kusaidiwa na meneja wake na akaongeza kwamba akipata milioni 6 anawekeza milioni 4 kwenye muziki huku akichukua milioni mbili kama faida ya kazi yake.





Licha ya kuzidi kutamba na kuonekana msanii wa kuigwa nchini Burundi, Gaga Blue alitoa donge kwa msanii mmoja wa Burundi bila kumtaja jina na kusema kuwa "Kuna msanii mkongwe Burundi ila hana mpango wowote kwenye muziki wakati pesa za show anazidi kuzipata ila ukitizama muziki wake hauna thamani yoyote."

Baadhi ya wafuatiliaji wa karibu wa muziki wa Indundi Music wanadai kauli hiyo ya Gaga Blue imemlenga msanii mwenzie Mugani Desire Big Fizzo jambo ambalo wengi wao kuhisi labda kutatokea utofauti wa ki kazi kati ya wawili hao.




0 comments: